Maonesho ya Nanenane 2025, Dodoma — Ushiriki wa Baraza la Masoko ya Mitaji (CMT)
Baraza la Masoko ya Mitaji ipo Dodoma kwa ajili ya Maonesho ya Nanenane yanayoendelea kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti 2025. Tupo ndani ya Banda la Academic and Research Institutions, tukitoa elimu kuhusu kazi zetu na namna tunavyosaidia kulinda haki za wawekezaji katika masoko ya mitaji.
Tunawahudumia wananchi kwa lugha rahisi, tukieleza:
- Tunachofanya kama Baraza
- Umuhimu wa uwazi na haki katika uwekezaji
- Jinsi ya kufikisha malalamiko kuhusu masuala ya masoko ya mitaji
Kaulimbiu ya mwaka huu ni:
“Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025”
kauli ambayo inaendana na dhima yetu ya kuimarisha mazingira ya uwajibikaji na uaminifu kwenye sekta ya fedha.
Njoo ututembelee, ujifunze, ulize maswali, na ujionee namna taasisi za umma zinavyofanya kazi kwa ajili ya wananchi!
Tupo kwa ajili yako. Karibu sana!